Jumapili 1 Novemba 2026 - 09:00
Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Hawza/ Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), ameshiriki katika hafla ya kuwavisha vilemba wahitimu wa masomo ya awali ya Hawza katika chuo cha Hawzat Al Qaim kilichopo jiji Tanga Tanzania, kinachosimamiwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, Tawi la Tanga.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo iliyofanyika jana tareh 31 Oktoba 2026, ilikuwa sehemu ya mahafali ya 14 ya chuo hicho, ambapo wanafunzi waliohitimu hatua ya awali ya masomo yao ya Hawza walivishwa vilemba kama ishara ya kukamilisha hatua hiyo muhimu ya kielimu na kidini.

Vilemba hivyo vinaashiria hatua mpya katika safari ya wahitimu hao ya kutumikia dini na jamii, huku vikiwakumbusha wajibu na dhamana kubwa inayowakabili katika kuendeleza elimu ya dini, kusimamia maadili ya Kiislamu na kuwaongoza waumini kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Jalala aliwapongeza wahitimu kwa kufikia hatua hiyo na kuwasisitiza umuhimu wa kujijenga katika misingi mitano muhimu ambayo kila mwanachuoni na mtafutaji wa elimu ya dini anapaswa kuizingatia katika maisha yake ya kila siku.

Misingi hiyo ni pamoja na kuswali swala kwa wakati wake, kudumisha swala za usiku, kusoma Qur’an Tukufu mara kwa mara, kuwa na tabia njema, pamoja na kuwa wakweli na waaminifu katika maneno na matendo yao.

Alieleza kuwa misingi hiyo ni miongoni mwa nguzo muhimu zinazomsaidia mwanachuoni kujijenga kiroho, kimaadili na kitabia, na kwamba elimu ya dini haipaswi kubaki katika kiwango cha maarifa na nadharia pekee, bali inapaswa kudhihirika kupitia matendo, mwenendo na namna mtu anavyoishi na watu wengine.

Aidha, aliwakumbusha wahitimu kuwa jukumu la mwanachuoni halikomei katika kujifunza na kupata maarifa ya kidini, bali linahusisha pia kuyafanyia kazi yale aliyojifunza, kuyafikisha kwa wengine na kuwa mfano mwema katika jamii.

Alisisitiza kuwa tabia njema, ukweli na uaminifu ni sifa zinazopaswa kuambatana na elimu ya dini, kwani mwanachuoni anapokuwa na maadili mema, huwa na nafasi kubwa ya kuwa na ushawishi chanya katika jamii na kuwavutia watu kupitia mwenendo wake.

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Awavisha Vilemba Wahitimu wa Hawzat Al Qaim Tanga/ Asisitiza Misingi Mitano ya Maisha ya Mwanachuoni

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha